Wakatazwa kuingia kwenye ndege, kisa HIV


Ndege ya shirika la ndege la China 

Abiria wawili wa china waliokuwa wakisafiri na ndege ya shirika la ndege la China (China Airline), wameamua kulipeleka shirika hilo mahakamani kwa kile walichokieleza kuwazuia kusafiri na shirika hilo eti tu kwasababu walikua wanaishi na virusi vya ukimwi HIV.

Hata hivyo inaelezwa kwamba abiria hao si mara ya kwanza kusafiri na China Airline kutoka kaskazini mwa mji wa Shenyang katika kipindi cha machipuko ,wakati huu sasa shirika hilo la ndege lilipoamua kughairisha safari za abiria hao.

Masharti ambayo abiria hao wameyatoa Kufuatia kughairishwa kwa safari hiyo,shirika hilo la ndege litalazimika kuomba radhi na kulipa fidia ya dola za kimarekani elfu nane .Mahakama katika mji wa Shenyang imeipokea na kukubali kesi hiyo ya kwanza na ya kipekee nchini China.

Viongozi wa serikali kutoka China wamesema kua wamejitahidi kujaribu kupunguza historia ya muda mrefu ya unyanyapaa kwa wanaoishi na virusi vya HIV na ukimwi
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Karibu tena..wasiliana nasi kwa simu namba 0758059936

Chapisha Maoni

 
Top