31 wafariki kutokana na Ebola DRC
2 Septemba, 2014 - Saa 12:22 GMT
Shirika la afya duniani
likishirikiana na wizara ya afya katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo
imesema kuwa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini humo umewaua watu 31.
Maafisa wanasema kuwa eneo hilo limewekwa karantini na zaidi ya watu 50 wanapokea matibabu baada ya kuambukizwa maradhi hayo.
Takriban watu 200 wanachunguzwa. Wizara ya afya mjini Kinshasa imesisitiza kuwa mlipuko wa homa hiyo haihusishwa na mlipuko wa Ebola uliotikisa kanda ya Afrika Magharibi ambako zaidi ya watu 1500 wamefariki.
Chapisha Maoni