|
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga bibi Annarose Nyamubi akimshukuru mwandishi wa habari bi Elif Esma kutoka nchini Uturuki kwa kutoa msaada wa magororo 253 katika kituo cha walemavu wa ngozi Alibino .Mkuu huyo wa wilaya alisema kituo hicho kinakabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo chakula na kwamba matatizo yote hayo yamesababishwa na halmashauri za wilaya zilizoleta watoto wenye ulemavu katika kituo hicho na kushindwa kuchangia shilingi 2,500 kwa siku kwa kila mtoto kwa ajili ya chakula na makazi bora kama yalivyokuwa makubaliano ya wakati wa kuanzisha kituo hicho miaka kadha iliyopita baada ya kuzuka kwa wimbi la ukatili wa walemavu wa ngozi. |
|
Mwandishi wa habari bi Elif Esma akimkabidhi dawa ya meno mtoto mwenye ulemavu wa ngozi |
|
Walemavu wa ngozi wakipokea misaada ya dawa na magodoro |
|
Add caption |
Mwandishi huyo wa habari akiwa mwenye tabasam baada ya kukamilisha dhamila yake ya kutoa msaada wa magodoro na kukarabati mabweni 6 kwenye kituo hicho.Hata hivyo alitoa wito kwa Serikali na watanzania kujenga utaratibu wa kukisaidia kituo hicho na kueleza kuwa wageni kama yeye ni wakupita tuu.
Chapisha Maoni