Mkuu wa mkoa wa Shinyanga bw Ally Nassoro Rufunga akifungua mkutano wa ushawishi wa viongozi na wadau wa mpango wa huduma rafiki ya afya ya uzazi kwa vijana mkoani Shinyanga.Katika ufunguzi wa mkutano huo bw Rufunga alisema mkoa wake unaongoza kwa asilimia 59 ya ndoa za utotoni na kutoa wito kwa wazazi na walezi kulitazama jambo hilo kwa vijana wao ili waweze kuwa na afya njema.alisema wasichana wa umri wa kati ya miaka 15 hadi 19 wamekwishaolewa mkoani Shinyanga.pia  mkoa wake unakadiliwa kuwa na vijana wapatao 625,125 mwaka 2013.na wengi wao hawana elimu ya afya ya uzazi na kwamba miongoni mwa changamoto ni upungufu wa vituo vya tiba na asilimia 75 watumishi watoa huduma awajapatiwa mafunzo ya utoaji wa huduma rafiki kwa vijana.

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Karibu tena..wasiliana nasi kwa simu namba 0758059936

Chapisha Maoni

 
Top