Itachukua miezi sita kudhibiti Ebola
15 Agosti, 2014 - Saa 14:23 GMT
Mkuu wa shirika la madaktari
wasio na mipaka la Medicins Sans Frontieres, amesema kuwa itachukua
miezi sita kuweza kudhibiti janga la Ebola katika mataifa ya Afrika
Magharibi.
Bi Lui aliongeza matabibu 80 wamefariki kutokana na ugonjwa huo, huku watu wengine 170 wakiambakizwa na kwamba nyingi ya vituo vya afya vimefurika wagonjwa wa Ebola.
''Ikiwa hatutapambana na ugonjwa huo nchini Liberia,basi itakuwa vigumu kuudhibiti katika kanda nzima ya Afrika Magharbi,'' alisema Bi Lui.
Mifumo ya afya katika neo la Afrika Magharibi inakabiliwa na hali ngumu wakati huu wa mlipuko wa Ebola.
Ebola huambukizana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine, kupitia maji maji ya mwili au damu.
Dalili kama za mafua zinaweza kusababisha mtu kuvuja damu kutoka kwenye sehemu zake za mwili kama vile masikioni, mapuani, machoni na ndani ya mwili na kusababisha viungo vya mwili kutofanya kazi.
Chapisha Maoni