Timu ya soka ya Stend ya Shinyanga imeichapa timu ya soka ya polisi Dodoma mabao 2 kwa 0 katika mchezo wa ligi daraja la kwanza kundi c mabao ya timu hiyo yalifungwa na wachezaji Husen  Masomo dk ya kwanza ya mchezo  na bao la pili lilifungwa Samwel Nyamba dk ya 90 .Timu hiyo ya Stend ambayo ilikuwa mabingwa wa ligi mpya ya mikoa inalelewa na vijana wanakatisha tiketi katika Stend ya mabasi mjini Shinyanga .Jambo ambalo kwa wakazi wa mkoa wa Shinyanga wamekuwa wakitafakali kwa kina uwezo wa vijana hao kuwa na timu inayofanya vizuri.Hata hivyo ni wajibu wa wakazi wa mkoa huo kuunga mkono juhudi za vijana hao kwa kuichangia timu hiyo inayoutangaza mkoa wa Shinyanga.

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Karibu tena..wasiliana nasi kwa simu namba 0758059936

Chapisha Maoni

 
Top