June 15, 2025 11:17:08 PM Menu


BBC navigation


WHO:Hofu ya 20,000 kuambukizwa Ebola


Mawaziri wa afya wa Afrika Magharibi wanakutana Ghana kutafita njia za kupambana na Ebola
Shirika la afya duniani WHO limeonya kuwa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola huko Afrika magharibi huenda ukasambaa na kuwaambukiza zaidi ya watu 20,000 kabla haujadhibitiwa.

Kwa sasa idadi ya waliothibitishwa na kuorodheshwa kuambukizwa ni elfu 3 ingawaje inashukiwa kuna wengi wengine ambao hawajajulikana.

Zaidi ya watu 1500 wamefariki kutokana na mlipuko wa sasa wa Ebola wengi wao wakiwa ni wa kutoka Liberia,Sierra Leone na Guinea.

Mkurugenzi wa WHO katika kanda hiyo - Dr Lious Sambo - ameeelezea jinsi wafanyikazi katika kliniki za wagonjwa wanavyo'ng'ang'ana wakijaribu kukabilianana na janga hilo la Ebola.

Wauguzi ni wachache ilihali wanapaswa kusaidia haraka inavyowezekana
Wagonjwa watano wa Ebola pia wamefariki Nigeria .

Mawaziri wa afya katika eneo hilo la Afrika magharibi wanakutana nchini GHana kujadili janga hilo.
Mkurugenzi wa MSF huko Liberia, Brice de la Vigne, ameiambia BBC vitanda zaidi ya elfu vinahitajika huko Liberia kwa minajili ya kuwatenga wagonjwa wa Ebola.
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Karibu tena..wasiliana nasi kwa simu namba 0758059936

28 Aug 2014
Next
FIFA:Platini asema hatampinga Blatter
Previous
Swahili Kwenye simu Matangazo Spika ahusishwa na kashfa ya kuwauza watoto 28 Agosti, 2014 - Saa 12:23 GMT Facebook Twitter Google+ Tuma kwa rafiki yako Chapisha Spika Hama Amadou alitoroka baada ya kuhusishwa na kashfa ya kuwauza watoto Spika wa bunge la Niger ametoroka nchini humo baada ya kamati ya bunge hilo kuafikia kukamatwa kwake kuhusiana na kashfa ya kuwauza watoto. Hama Amadou, ambaye tayari ameelezea azma yake ya kugombea urais mwaka 2016, anasema kuwa madai hayo dhidi yake yamechochewa kisiasa. Taarifa zinazohusiana Afrika, afrika magharibi Mke wa pili wa spika huyo na watu wengine 16 walikamatwa mwezi Juni baada ya kutuhumiwa kuwauza watoto wachanga Kusini Mashariki mwa Nigeria. Watoto hao huuzwa kwa maelfu ya dola kila mtoto. Mwandishi wa BBC nchini Niger anasema kuwa kesi hiyo imetoa fursa tosha kwa chama tawala kumuondoa Bwana Amadou kutoka katika chama hicho tangu kukosana na muungano tawala. Kashfa hii pia imewashtua wengi katika nchi hiyo yenye idadi kubwa ya waumini wa kiisilamu hasa kwa kuwa ni kosa kuonyesha kuwa watoto walioasiliwa na wako binafsi. Imeripotiwa kuwa baadhi ya wanawake walidai walikuwa wajawazito na kwenda Nigeria kabla ya kurejea na watoto wao. Kamati kuu ya bunge la taifa ambalo linamjumuisha naibu spika na wakuu wengine wa kamati nyinginezo, walikutana Jumatao, na kukubaliana kuwa polisi wanaweza kumkamata na kumhoji bwana Amadou kuhusiana na tuhuma hizo. Wanasiasa sita wa upinzani walikataa kuhudhuria vikao hivyo ingawa idadi ya wabunge waliofika ilitosha kutoa uamuzi. Kikao kamili cha bunge kitahitajika kufanyika ili kuondoa uwezekano wa bwana Amadou kushitakiwa. Inadaiwa watoto 30 wameuzwa katika kashfa hii ambayo imehusisha kutengeza stakabadhi bandia na kubadili vyeti vya kuzaliwa vya watoto waliouzwa.

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top