FIFA:Platini asema hatampinga Blatter
Rais wa shirikisho la soka barani Uropa Uefa Michel Platini hatompinga Sepp Blatter katika kura za kuwania rais wa FIFA mwakani.
Platini amewambia wajumbe hao 54 kuwa licha ya yeye kutaka kuwe na ''hewa safi katika FIFA'' anapendekeza kujitolea kimasomaso katika uongozi wa UEFA.
Mwanakamati wa Fifa Michel D'Hooghe alisema '' ni jambo la kutoa moyo kwani inamanisha kuwa mwaka huu hatutakuwa na ubishi kati ya UEFA na FIFA''
Blatter, 78,ameongoza FIFA tangu mwaka wa 1998, lakini amekumbwa na upinzani mkubwa baada ya kuibuka tuhuma za hongo katika uwenyeji wa kombe la dunia la mwaka wa 2022.
Kujiondoa kwake sasa kunamwacha Blatter akikabiliana na aliyekuwa katibu mkuu wa FIFA wa zamani Jerome Champagne.
Wagombea wanapaswa kutangaza niya yao kuanzia Januari 2015 hata hivyo Platini atalazimika kusubiri hadi baada ya miaka mingine minne ilikuwania urais mwaka wa 2019.
Platini, aliiongoza Ufaransa kutwaa taji la Uropa mwaka wa 1984.
Ameiongoza Uefa tangu mwaka wa 2007.
Anatarajiwa kuiongoza Ufaransa kupanga na kuandaa mchuano wa Euro 2016 mbali na makala ya mwaka wa Euro 2020 .
Chapisha Maoni