Serikali nchini yashauriwa kuwekeza nguvu zake katika mchezo wa masumbwi kama ilivyowekeza katika michezo mingine ikiwemo Soka,Hayo yamesemwa na Mwanamasumbwi wa Kimataifa Shija Emmanuel wakati alipokua akiongea na Shalley Habari mjini Shinyanga.

Bondia huyo wa kimataifa ambae ni mzaliwa wa Shinyanga alisema kwa muda mrefu sasa serikali imekua ikitupia jicho katika mchezo wa Soka wakati nchini kuna michezo mingi ikiwemo Masumbwi mchezo ambao umekua ukifanya vizuri Kimataifa.

Mchezo huo wa masumbwi ukiwezeshwa unaweza kuibua vipaji vingi na kuliletea Taifa mafanikio makubwa ikiwemo kuongeza pato la Taifa.Bondia huyo alisema nchi zilizoendelea mchezo wa masumbwi umekua ni kivutio kubwa kwa mashabiki na wawekezaji wamekua wakijitokeza kwa wingi kusapoti mchezo huo tofauti na hapa nchini.



Bondia Shija akiwa katika moja ya sehemu ya mazoezi yake huko Ughaibuni.
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Karibu tena..wasiliana nasi kwa simu namba 0758059936

Chapisha Maoni

 
Top