Ebola bado ni Tishio
Wakati ugonjwa wa Ebola
ukiendelea kuumiza vichwa vya wanasayansi walio wengi juu ya namna ya
kuboresha tiba ya majaribio ya Zimapp,mengi yameendelea kuibuka juu ya
ugonjwa huu.
Kuna taarifa kua madaktari wasio na mipaka(
medical charity Médecins Sans Frontières ) wamekosoa uwajibikaji wa
umoja wa mataifa pamoja na shirika la afya duniani WHO suala la ugonjwa
wa Ebola huko Africa Magharibi.Mkurugenzi wa madaktari hao wasio na mipaka Brice de la Vigne,ameeleza namna ugonjwa wa Ebola na unavyoenezwa unavyochukuliwa ni sawa na hakuna juhudi yoyote ama kwakifupi ni sifuri kiutendaji kwa wadau hao wakuu .
Shirika hilo la Afya ulimwenguni W.H.O limetoa takwimu ya watu waliopoteza maisha kutokana na ugonjwa wa Ebola Africa Magharibi kwamba kufikia sasa inazidi kuongezeka na kufikia zaidi ya wafu elfu kumi na watatu.
Chapisha Maoni