Kikongwe mwenye umri wa miaka 62 Raheli Jilungu mkazi wa kijiji cha Mishepu wilayani Shinyanga aliuawa kwa kukatwa shingo na mtuhumiwa aliyetambulika kwa jina la Maganga Fuja akiwa na wenzake
watatu .Chanzo cha mauaji hayo ni imani potofu za  kishirikina 
Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka kati ya 10 na 12 alikutwa kwenye vichaka katika kijiji cha Betende kata ya Kizumbi manspaa ya Shinyanga akiwa amefariki huku mwili wake ukiwa umetobolewa sehemu mbalimbali sanjali na kufanyiwa vitendo vya ukatili .
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga kamishina msaidizi Justus Kamugisha atoa wito kwa wakazi wa mkoa wa Shinyanga kupambana na vitendo vya mauaji ya vikongwe.Kamugisha alisema kazi kubwa hivi sasa kwa upande wake kuhakikisha mauaji yanakoma mkoani Shinyanga.alisema ufanisi wa mapambano hayo  yanategemea  ushirikiano kutoka kwa wakazi wa mkoa wake kwa kutoa taarifa za wausika wa mauaji hayo.alisema mauaji hayo yamekuwa na mtandao mkubwa wakiwemo ndugu wa marehemu wanaofanyiwa vitendo hivyo.
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Karibu tena..wasiliana nasi kwa simu namba 0758059936

Chapisha Maoni

 
Top