Mwandishi wa Habari auawa Syria

 
James Foley enzi za uhai wake akiwa na vitendea kazi vyake.

Kikosi cha kiislam cha kijeshi chenye msimamo mkali kimeachilia video inayoonesha mauaji ya mwandishi habari mwenye asili ya Marekani. James Foley alipotea tangu alipokamatwa mateka na kushikiliwa nchini Syria miaka miwili iliyopita na sasa ameuawa.

Ikulu ya Marekani imesema inaifanyia uchunguzi wa kina video hiyo na ikithibitika kwamba mwandishi huyo wa habari ni wa taifa hilo ,serikali ya Marekani itataka ufafanuzi wa kina ilikuaje na kwanini James Foley auawe.

Katika mtandao wa kijamii wa Facebook familia ya mwandishi huyo iliandika kuwa’tunajua kwamba wengi wenu mnasubiri uthibitisho ama majibu ya maswali yenu,tafadhalini muwe watulivu mpaka nasi sote tupate taarifa tunazo tamia,na tunaomba muendelee kumbumbuka Foleys na kumwombea kila siku.’

Katika video hiyo iliyobeba ujumbe unaosomeka kua ujumbe kwa Marekani,mwandishi huyo pia alionekana akiwa chini ya ulinzi wa mtu aliyekua amevalia kinyago usoni,askari huyo alikua aku akizungumza ndani ya lafidhi yenye athari za Uingereza,akisema kua kifo cha mwandishi huyo ni matokeo ya mashambulizi ya magurunedi yalowalenga wa Iraq.
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Karibu tena..wasiliana nasi kwa simu namba 0758059936

Chapisha Maoni

 
Top