Mwafrika mwingine auawa Missouri
Mauaji mengine ya raia wa
kiafrika yaliyofanywa na polisi katika eneo la St Louis yameongeza hali
ya wasiwasi na vurugu katika eneo hilo ambalo kwa takriban siku 11 sasa
kumekuwa na vurugu kutokana na mauaji yaliyotokea awali.
Mwanasheria mkuu wa Marekani Eric Holder anatarajiwa kutembelea eneo la Ferguson jumatano wiki hii ili kujadili taaerifa rasmi za uchunguzi wa mauaji hayo.
Mwendesha mashitaka katika kesi ya mauaji ya ya Michael Brown leo amewasilisha ushahidi dhidi ya afisa anayedaiwa kuhusika katika mauaji ya Michael Brown.
Vurugu zimeendelea katika mji huo huku waandamanaji wanaopinga mauaji hayo wakiwa wamepakaa maziwa usoni kujikinga na mabomu ya machozi kufuatia waandamaji wawili kuathirika na mabomu hayo.
Chapisha Maoni