Wafanyakazi wa Banki ya NMB tawi la Manonga manspaa ya Shinyanga wametoa msaada wa vitendea kazi kwenye Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga kufuatia ajali mbili mfululizo ambazo zimesababisha vifo vya watu 3 na wengine zaidi ya 90 kujeruhiwa.Meneja wa Banki hiyo bw Jemes Poneka alisema wafanyakazi wameguswa na matukio hayo ya ajali na kufikia hatua ya kuchanga fedha kwa ajili ya kununua vifaa ambavyo vitasaidia kuokoa maisha ya waanga wa ajali hizo.Kwa upande wake mganga mfawidhi wa Hospitali hiyo Dr Mlekwa amewapongeza wafanyakazi wa Banki ya NMB kwa kuguswa na matukio hayo ya ajali na kueleza bayana kwamba msaada huo umefika kwa wakati na kutoa wito kwa taasisi zingine kuiga mfano huo.
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Karibu tena..wasiliana nasi kwa simu namba 0758059936

Chapisha Maoni

 
Top