Timu ya soka ya Stend ya Shinyanga imeendelea kukaa kileleni mwa ligi daraja la kwanza kundi c baada ya kuifunga timu ya soka ya Polisi Mara goli 1 mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Karume mjini Musoma mwishoni mwa waki hii.Mchezo huo ulitawaliwa na fujo za mashabiki na kusababisha jeshi la Polisi kukabiliana na mashabiki hao .Hata hivyp hadi dakika 90 za mchezo huo zinamalizika fujo ziliendelea kutanda hatua ambayo jeshi la Polisi mkoani humo kuweka ulinzi katika msafara wa timu ya Stend hadi nje ya mji huo wa Musoma.Kwa matokeo hayo timu ya Stend inaongoza kwa pointi13 ikifuatiwa na Kanembwa JKT ya Kigoma 9,Mwadui ya Shinyanga 8,Polisi Tabora 6,Pamba ya Mwanza 4 ,wakati Toto ya Mwanza 3 na Polisi Dodoma pointi 3
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Karibu tena..wasiliana nasi kwa simu namba 0758059936

Chapisha Maoni

 
Top