Mkuu wa wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu bw Erasto Sima ametoa shutuma nzito kwa Bohari ya dawa MSD kwa kushindwa kusambaza dawa kwenye Hospitali za wilaya na mikoa na kusababisha kutokea kwa vifo vya wagonjwa kwa sababu ya ukosefu wa dawa.Mkuu huyo wa wilaya alitoa shutuma hizo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upimaji wa macho wilayani humo.alisema pamoja na Halmashauri za wilaya kuwa na fedha za kununulia dawa lakini MSD wameshindwa kutoa huduma hiyo kwa wakati.Kufuatia hali hiyobw Sima alitoa wito kwa wizara ya Afya kujipanga upya kwa kutoa fursa zaidi kwa wasambazaji wengine wa dawa ili pawepo ushindani utakao leta tija tofauti na hivi sasa sheria inazitaka Halmashauri kununua dawa na vifaa tiba MSD pekee jambo ambalo kwa MSD wameshindwa kumudu mahitaji ya usambazaji wa dawa na vifaa.Alisema kutokana na hali hiyo baadhi ya wagonjwa wamekuwa wakipoteza maisha wilaya Bariadi kwa sababu ya kukosa huduma za tima.
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Karibu tena..wasiliana nasi kwa simu namba 0758059936

Chapisha Maoni

 
Top