Kikosi
cha wanamaji nchini Indonesia kikisali kabla ya kuanza zoezi la
kuitafuta Ndege ya AirAsia QZ8501 katika bandari ya Pangkal Pinang
kwenye kisiwa cha Sumatra.
Kufuatia kupotea kwa ndege ya
shirika la ndege la Asia ndege namba QZ8501At ,miili arobaini imeopolewa
kutoka baharini katika utafutaji wa mabaki ya ndege hiyo na utafutaji
unaendelea.
Miili hiyo ilionekana ikielelea karibu na taka za
bahari pwani ya Indonesia,eneo la Borneo moja ya eneo la utafutaji
mabaki ya ndege hiyo.Na taarifa kutoka serikali ya Indonesia
zimethibitisha kwamba miili hiyo inatoka katika ndege iliyopotea.
Ndege
hiyo aina ya Airbus A320-200,ilikuwa imebeba abiria mia moja na sitini
na wawili ikitokea Surabaya nchini Indonesia kuelekea Singapore,ilipotea
siku ya Jumapili.
Utafutaji wa mabaki ya ndege hiyo umeingia
katika siku ya tatu,na eneo la utafutaji limeongezwa na kufikia kanda
kumi na tatu hii inashirikisha nchi kavu na baharini.
Wakati wa
mkutano na waandishi wa habari uliooneshwa wazi kwenye runinga ya taifa
la Indonesia picha za taka bahari zilioneshwa zikiwa zimechanganyika na
mabaki ya miili ya abiria ikielea majini.
Ndugu wa mabaki hayo
walipoona picha hizo walipigwa na fadhaa kuu na walionekana kushtushwa
na picha hizo.Baadaye askari wa majini nchini Indonesia wameeleza kuwa
miili hiyo arobaini iliopolewa na meli ya kivita .
Mkurugenzi
mtendaji wa AirAsia Fernandes ali ingia katika mtandao wa twitter na
kueleza huzuni yake kwa ndugu waliopoteza ndugu zao katika ndege QZ
8501. Na kwa niaba ya shirika la ndege la AirAsia ametuma salamu za
rambi rambi .
Utafutaji miili na mabaki ya ndege hiyo unashirikisha meli thelathini,ndege kumi na tano na chopa saba.
Chapisha Maoni