VITUKO SHY



Hii ni kali ya mwaka iliyojitokeza katika eneo la Kambarage Manispaa Shinyanga kwenye Bar moja maarufu jina kupuni.

Ambapo watu waliokuwepo kwenye Bar hiyo walipigwa butwaa baada ya kuona jeneza likiingizwa ndani ya Bar hiyo.

Kama picha inavyoonekana Bwana huyu jina kapuni akiingia na jeneza na kumtaka mmoja wa wahudumu wa Bar hiyo aingie ndani ya jeneza hilo aondoke nae baada ya kukataa kumpa Bia mbili alizonunuliwa na rafiki yake.

Inasemekana kuwa jamaa huyo aliyebeba jeneza alitinga ndani ya Bar hiyo na mmoja kati ya rafiki zake na kumuagizia bia mbili ambazo inadaiwa kuwa muhudumu wa meza hiyo alikataa kumpatia bia hizo.

Ndipo jamaa huyo ambae ni mbeba mizigo maarufu eneo hilo akaenda kubeba jeneza amabalo alilifata jirani na eneo hilo yanapotengenezwa na kuja nalo mpaka katika Bar hiyo na kusababisha watu waliokuwepo katika eneo hilo kukimbia kwa maajabu haya.

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Karibu tena..wasiliana nasi kwa simu namba 0758059936

Chapisha Maoni

 
Top