Watu 63 wamenusurika katika ajari ya basi la kampuni ya Najmunisa lililopinduka jumatatu wiki hii kwenye eneo la Usanda wilayani Shinyanga likitokea jijini Mwanza kwenda jijini Dar sallam

Basi lenye namba T242 BRJ likiendeshwa na dereva bw Dikson Paulo lilipata ajari hiyo kufuatia guludumu la mbele kupasuka na kusababisha kuangauka kutokana na mwendo kasi katika ajari hiyo akuna mtu aliyepoteza maisha

Majeruhi wa ajari hiyo 47 wanatibiwa kwenye hospitari ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga  Jeshi la polisi mkoani Shinyanga linaendelea na uchunguzi wa ajari hiyo.

Hata hivyo eneo hilo la usanda limekuwa sugu kwa matukio ya ajari za barabarani mara kwa mara na kusababisha vifo vya watu na ulemavu wa kudumu
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Karibu tena..wasiliana nasi kwa simu namba 0758059936

Chapisha Maoni

 
Top