Watu 3
wamekufa na wengine zaidi ya 47 wamejeruhiwa baada ya gari walilokuwa
wakisafiria kwenda mnadani kupinduka wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga.
Ajari hiyo
imetokea asubuhi katika eneo la uchunga wilayani humo baada ya gari
hilo haina ya fuso namba T680 ARL kuacha njia na kupinduka.
Chanzo cha
ajari hiyo ni mwendo kasi na derava wa gari hilo aliyetambulika kwa jina la
Shija Ngassa amekimbia baada ya ajari
hiyo
Ajari hiyo
ya fuso imesababisha vifo vya watu watatu ambapo moja ametambulika kwa jina la
Difa Shimo mili ya marehemu imehifadhiwa
kwenye hospitali ya mkoa wa Shinyanga.
Kamanda wa
polisi wa mkoa wa Shinyanga kamishina msaidizi wa polisi Jastus Kamugisha amethibitisha
kutokea kwa ajari hiyo.
Kamugisha
amesema jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo pamoja na
kumsaka dereva wa gari hilo sanajali na kutoa onyo kwa wafanya biashara wa
minadani kuacha kupanda magari ya mizigo
Chapisha Maoni