Mtuhumiwa aliyekuwa akikabiliwa na
kesi za ubakaji na kulawiti watoto katika Manispaa ya Shinyanga amehukumiwa kifungo cha maisha
gerezani kwa kesi tatu tofauti.
Mtuhumiwa huyo
Jacob Mayani au maarufu kwa jina la Boy mwenye umri wa miaka 28 mkazi wa
manspaa ya Shinyanga amehukumiwa vifungo
vitatu vya maisha kwenye MAHAKAMA ya Hakimu mkazi Mfawidhi Shinyanga.
Jacob Mayani
ambae alituhumiwa kuhusika na matukio
tofauti ya ubakaji na kulawiti watoto chini ya maiaka 10 sanjari na kuwatoboa
macho amejikuta akiishia gerezani.
Kabla ya
kutolewa hukumu ya tatu ya kifungo cha maisha wiki hii na mh Hakimu mkazi
mfawidhi John Chaba tayari mtuhumiwa huyo alikua ameshahukumiwa vifungo vingine
viwili vya maisha kwa kesi za ubakaji na
ulawiti
.
Akisoma
hukumu hiyo Hakimu Chaba amesema ameridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa
mashitaka dhidi ya mtuhumiwa huyo na adhabu hiyo itakua fundisho kwa Mayani na
wengine.
Awali
ilidaiwa na upande wa Mashitaka ukiongozwa na wakili wa serikali Salome Mbuguni
kwamba Mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo
February 12 mwaka jana majira ya saa kumi jioni katika kijiji cha Mwamashele
Kizumbi Manispaa ya Shinyanga kwa kumbaka mtoto huyo wa darasa nne.
Upande huo wa mashitaka ulidai kwamba mtoto
huyo alikua ametumwa mandazi na mama yake mdogo ndipo alipokutana na mtuhumiwa
njiani na kumrubuni aende nae akampatie mzigo wa bibi yake ndipo alipofanya
kitendo hicho.
Mbali na
vifungo hivyo vitatu vya maisha gerezani
Mayani anakabiliwa na kesi ingine ya kubaka pamoja na tuhuma ya kutoboa
macho watoto kesi ambayo itasikilizwa na mahakama Kuu baada ya upelelezi
kukamilika
Shalley habari ilipata fursa ya kuongea na mwanaharakati
wa kutetea haki za watoto Mkoani Shinyanga bw John Shija ambae anaunga mkono adhabu hizo.
Mwaka 2013
paliibuka matukio ya ubakaji na kulawitiwa
watoto pamoja na kutobolewa macho katika
manspaa ya Shinyanga Jambo ambalo liliwaweka wazazi na watoto katika hofu
kubwa.
Chapisha Maoni