Katika hali isiyokuwa ya kawaida wachimbaji wadogo kwenye machimbo ya Mwashina wilayani Nzega mkoani Tabora watakiwa kuondoka eneo hilo tangu leo.Habari kutoka katika machimbo hayo zinasema kuwa tayari askari polisi wapo eneo hilo hata hivyo wachimbaji hao wanasema kuwa kuwafukuza kwenye machimbo hayo ni kuwanyima ajila na kwamba tayari walikuwa wametumia nguvu na fedha katika uchimbaji. Wakazi wa mji wa Nzega wamepokea kwa masikitiko makubwa kauli hiyo ya Serikali ya kuwaondoa wachimbaji hao ambao walikuwa wanakuza uchumi wa mji huo na kuitaka Serikali kusitisha zoezi hilo kwa manufaa ya wakazi wa Nzega.
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Karibu tena..wasiliana nasi kwa simu namba 0758059936

Chapisha Maoni

 
Top