Hali ni tete  kwa wakulima wa zao la mtama katika wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga ambapo ndege aina ya kwelea kwelea wanashambulia zao hilo kwa kasi hivyo kutishia balaa la njaa kwa wakazi wa eneo hilo ambao wameliona zao hilo kama mbadala wa mahindi ambayo yamekuwa yakikauka kutokana na uhaba wa mvua.
Pichani ni afisa kilimo wa kituo cha kilimo ch mwamala kijiji cha Bubinza kata ya Mwamashele wilayani Kishapu Simon Bitege akitumia njia za asili kufukuza kwelea kwelea kutokana na kukosekana kwa ndege ya kuangamiza ndege hao.
Tanzania haina ndege ya kuangamiza na hivyo kutegemea ndege ya Shirikisho ambayo ipo nchini Ethiopia na kuwa changamoto kubwa kwa wakulima nchini.
Wakulima wa Tanzania wamekuwa na mtazamo tofauti juu ya mazao yao kushambuliwa na ndege kila mwaka na kuitaka serikali kununua ndege ya kuangamiza wadudu na ndege ili kwenda sambamba na mpango wa kilim kwanza.
Hata hivyo baadhi ya viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu akiwemo mkurugenzi wa wilaya hiyo  Ruchius Bilakwata,afisa kilimo wa wilaya Godwin Everygist pamoja na afisa kilimo wa kituo cha Mwamala Simon Bitege wanaelezea ukubwa wa tatizo hilo
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Karibu tena..wasiliana nasi kwa simu namba 0758059936

Chapisha Maoni

 
Top