Kauli hiyo imetolewa na mkurugenzi wa shirika lisilokuwa la kiserikali la Egpahi bw Laurean Rubambwa linalopambana na maambukizo ya ugonjwa wa ukimwi nchini chini ya mpango wa Rais Mstaafu wa Marekeni mh bush wakati wa ufunguzi wa kituo cha tiba na vipimo kwa waathirika wa ukimwi wilayani Mbogwe mkoani Geita. Mkurugenzi huyo alisema kwa sasa virus vya ugonjwa wa ukimwi vinakabilika kwani kuna huduma ya dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo na kutoa wito kwa wa Tanzania kujenga utaratibu wa kupima afya zao sanjali na kuhakikisha wakina mama wajawazito wanapimwa afya zao.alisema mama mjamzito ambaye atabainika ameambukizwa virus vya Hiv atapatiwa dawa za kudhibiti maambukizo ya virus hivyo kwenda kwa mtoto.alisema mpango huo wa dawa za kudhibiti maambukizo ya virus vya ukimwi kutoka kwa mama mjamzito umeonyesha mafanikio makubwa hapa nchini.
|
Chapisha Maoni