Ujenzi wa jengo la Mahakama kuu kanda ya Shinyanga umesimama kwa muda mrefu na kusababisha kuwa makazi ya vibaka na mifugo.Habari zinaeleza kwamba kusimama kwa jengo hilo umesababishwa na ukosefu wa fedha za kumalizia ujenzi .Hata hivyo wakazi wa mkoa wa Shinyanga wamekuwa na mtazamo tofauti kuhusu kusimama kwa ujenzi huo ukizingatia mkoa wao unakesi nyingi ambazo zinatakiwa zisikilizwe na mahakama kuu.Wameitaka Serikali kupitia wizara usika kumalizia ujenzi huo ambapo fedha za walipa kodi tayari zimetumika kwa kiasi kikubwa.
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Karibu tena..wasiliana nasi kwa simu namba 0758059936

Chapisha Maoni

 
Top