Ebola bado tishio Sierra Leone
Maafisa
wa Afya nchini Sierra Leone wamegundua miili kadhaa katika maeneo ya
mgodi wa Almasi, na kusababisha hofu kuwa pengine ugonjwa wa Ebola
haujaripotiwa ipasavyo
.
Shirika la afya duniani,WHO limesema
limebaini kisa hiki kipya mashariki mwa mji wa Kono, timu ya Wataalamu
imepelekwa Kono kufanya uchunguzi kuhusu uwepo wa ugonjwa wa Ebola.Watu 6,346 wamepoteza maish akutokana na ugonjwa huo na zaidi ya 17,800 wameathirika na Ebola.
Sierra Leone ina idadi kubwa zaidi ya Watu wenye Ebola Afrika Magharibi, ikiwa na Watu walioathirika 7,897 tangu kuanza kwa ugonjwa huo.
WHO imesema katika kipindi cha takriban siku 11 mjini Kono, Miili 87 ilizikwa.
Chapisha Maoni