Kilimo cha zao la tumbaku pamoja na kuchangia kwa asilimia kubwa ya uchumi wa wilaya ya Kahama lakini kimekuwa kikisababisha uhalibifu mkubwa wa mazingira.Mkuu wa wilaya hiyo bw Benson Mpesya alisema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti.alisema asilimia 75 ya mapato ya Halmashauri ya Ushetu yanatokana na zao la tumbaku huku asilimia zaidi ya 80 ya wakazi wa Ushetu wanategema kilimo cha zao hilo.Msimu uliopita wakulima wa zo hilo walinufaika na kitita cha fedha zaidi ya bilioni 10 sanjali na  Halmashauri ya Ushetu ikipata ushuru wa milioni 900 kutoka katika zao la tumbaku lakini kasi ya ukataji miti ni kubwa pamoja na mafanikio hayo ya kiuchumi.
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Karibu tena..wasiliana nasi kwa simu namba 0758059936

Chapisha Maoni

 
Top