Halmashauri za wilaya mkoani Shinyanga zenye watoto wenye ulemavu wa ngozi zaendelea kukaidi kuchangia fedha za chakula katika kituo maalum cha Buhangija kilichopo manspaa ya Shinyanga.Uchunguzi uliofanywa na Blog hii umebaini pamoja na kutokea tatizo la upungufu mkubwa wa chakula kwenye kituo hicho lakini hakuna Halmashauri iliyochukuwa hatua na kuacha mzigo huo kwa manspaa ya Shinyanga.Miaka kadhaa iliyopita wakati wa wimbi la ukatili dhidi ya walemavu wa ngozi kuibuka nchini mkoa wa Shinyanga ulianzisha kituo hicho kwa lengo zuri la kuwalinda walemavu hao.Miongoni mwa vyanzo vya fedha kwa ajili ya chakula na makazi bora ni kila halmashauri yenye mtoto kituoni hapo ichangie kiasi cha shilingi 2,500 kwa siku kwa mtoto mmoja. Lakini hadi leo zaidi ya shilingi milioni 160 zinadaiwa na mtoa huduma ya chakula na kusababisha kusitisha huduma hiyo jambo ambalo limesababisha tatizo la upungufu mkubwa wa chakula.
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Karibu tena..wasiliana nasi kwa simu namba 0758059936

Chapisha Maoni

 
Top