Mkuu wa wilaya ya Itilima Bibi Budala akipokea msaada wa vitabu na madawati na kusema kuwa vifaa hivyo vimekuja kwa wakati kwani wilaya yake inakabiliwa na upungufu mkubwa wa madawati. Tunaupungufu wa madawati 16,862 katika shule za msingi na sekondari tunawashukuru  kwa misaada yenu alisema. Hata hivyo siku ya leo tunaitumia kuzindua mfuko endelevu wa kukabiliana na tatizo la madawati. Alisema fedha ambazo zitapatikana zitatumika kutengenezea madawati wilaya yangu yenye kata 23 tutaandaa mpango wa kila kata kuchangia fedha ambapo kwa leo tumepata zaidi ya milioni moja na laki nne mwanzo ni mzuri, sanjali na kumushukuru mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Itilima Njaru Silanga kwa kuchangia  madawati 250, mabati 250 pamoja na saluji na kutoa wito kwa wadau wengine kuiga mfano huo.

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Karibu tena..wasiliana nasi kwa simu namba 0758059936

Chapisha Maoni

 
Top