Daktari aliyetibiwa na Zmapp aaga Liberia
Daktari mmoja kutoka Liberia ambaye aliambukizwa ugonjwa wa Ebola na kutibiwa na dawa ya ZMAPP ameaga dunia.
Kufikia sasa zaidi ya watu 1,400 wameaga dunia kutokana na homa hiyo ya Ebola katika ukanda wa Afrika Magharibi katika mataifa ya - Guinea, Liberia, Nigeria na Sierra Leone.hirika la Afya Duniani, WHO limesema kasi na kiwango cha milipuko hiyo hakijawahi kutokea hapo kabla.
Watu wanaokadiriwa kufikia 2,615 Afrika Magharibi wameambukizwa ugonjwa wa Ebola tangu uzuke mwezi Machi mwaka huu.
Kirusi cha Ebola
Hata hivyo dawa hiyo imeadimika kwa sasa.
Pia Jumapili, mfanyakazi wa afya wa Uingereza aliambukizwa ugonjwa wa Ebola nchini Sierra Leone na kurejeshwa Uingereza akisafirishwa na ndege ya jeshi la Uingereza, RAF.
Ni mgonjwa wa kwanza Mwingereza kuthibitishwa kuambukizwa virusi vya Ebola wakati wa mlipuko wa sasa wa ugonjwa huo.
Marekani imetuma vifaa vya tiba kusaidia kupambana na mlipuko wa Ebola nchini Liberia.
Watu kadha wamekufa katika kipindi cha mwezi uliopita baada ya kuugua homa isiyojulikana katika jimbo la Equateur katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Jumapili, Waziri wa Afya wa DR Congo Felix Kabange Numbi amesema watu wawili kati ya wanane waliopimwa ugonjwa Ebola wamethibitika kuambukizwa ugonjwa huo.
Ebola ilivyoenea Afrika
Ameiambia BBC kuwa eneo la karantini litawekwa katika eneo la kipenyo cha kilomita za mraba 100 katika eneo la Boende ambao wagonjwa wamegundulika.
Virusi vya ugonjwa wa Ebola kwa mara ya kwanza viligundulika nchini humo mwaka 1976 karibu na Mto Ebola.
Bwana Numbi amesema vipimo zaidi vinafanyika.
Jumamosi, bunge la Sierra Leone lilipitisha sheria mpya kuwa ni kosa la jinai kuwaficha wagonjwa wa Ebola.
Chapisha Maoni