Marekani yataka Iran ishiriki vita dhidi ya Dola la Kiislamu

Marekani inakiri kuwa hata adui mkubwa, Iran, ana wajibu mkubwa kwenye kulishinda kundi linalojiita "Dola la Kiislamu" ambalo limeshachukuwa eneo kubwa la mataifa ya Syria na Iraq.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry, akizungumza kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry, akizungumza kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Akizungumza kwenye kikao cha mawaziri wa nje wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Kerry alisema katika juhudi za pamoja za kimataifa dhidi ya kitisho cha kundi hilo, "takribani kila nchi ina jukumu la kutekeleza, ikiwemo Iran."

Wiki hii, Kiongozi Mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Ayatullah Ali Khamenei, alisema alikuwa amelikataa ombi la Marekani la kushirikiana nayo kwenye uwanja wa mapambano.

 Ingawa maafisa wa Marekani hawajathibitisha wala kukanusha kutuma ombi hilo, lakini kimsingi wamekuwa hawaichukulii Iran kuwa sehemu ya muungano wanaouunda kupambana na Dola la Kiislamu.

Wiki iliyopita, mwanadiplomasia mmoja wa ngazi za juu wa Marekani alisema lisingelikuwa jambo muafaka kuialika Iran kwenye mikutano inayojaribu kujenga muungano huo wa kimataifa kutokana na "kujihusisha kwa serikali ya Iran nchini Syria na kwengineko."

Kwa upande mwengine, Iran inaziunga mkono serikali za Iraq na Syria katika vita vyao dhidi ya kundi hilo la Dola la Kiislamu.
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Karibu tena..wasiliana nasi kwa simu namba 0758059936

Chapisha Maoni

 
Top