Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt Ntuli Kapologwe akizungumza na waandishi habari juu ya uvumi wa kuwepo kwa ugonjwa wa Ebola mkoani Shinyanga,alisema hakuna ugonjwa huo japokuwa siku ya Jumanne wiki hii katika hospitali ya mkoa alipokelewa mgonjwa aliyekuwa akitokwa damu jambo ambalo lilileta taharuki kwa wauguzi na madaktari lakini baada ya kufanyiwa uchunguzi ilibainika kuwa hakuwa na dalili zozote za ugonjwa huo.

Alisema idara yake imejipanga vyema kukabiliana na ugonjwa huo kwenye halmashauri zote za wilaya huku nguvu kubwa ikielekezwa wilaya ya Kahama ambayo ina mwingiliano wa raia kutoka nchi jirani ya Rwanda na Burundi.

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Karibu tena..wasiliana nasi kwa simu namba 0758059936

Chapisha Maoni

 
Top