Hali ni tete kwa
wakulima wa zao la mtama katika wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga ambapo ndege
aina ya kwelea kwelea wanashambulia zao hilo kwa kasi hivyo kutishia balaa la
njaa kwa wakazi wa eneo hilo ambao wameliona zao hilo kama mbadala wa mahindi
ambayo yamekuwa yakikauka kutokana na uhaba wa mvua.
Pichani ni afisa kilimo wa kituo cha kilimo ch mwamala
kijiji cha Bubinza kata ya Mwamashele wilayani Kishapu Simon Bitege akitumia
njia za asili kufukuza kwelea kwelea kutokana na kukosekana kwa ndege ya
kuangamiza ndege hao.
Tanzania haina ndege ya kuangamiza na hivyo kutegemea ndege
ya Shirikisho ambayo ipo nchini Ethiopia na kuwa changamoto kubwa kwa wakulima
nchini.
Wakulima wa Tanzania wamekuwa na mtazamo tofauti juu ya
mazao yao kushambuliwa na ndege kila mwaka na kuitaka serikali kununua ndege ya
kuangamiza wadudu na ndege ili kwenda sambamba na mpango wa kilim kwanza.
Hata hivyo baadhi ya viongozi wa halmashauri ya wilaya ya
Kishapu akiwemo mkurugenzi wa wilaya hiyo
Ruchius Bilakwata,afisa kilimo wa wilaya Godwin Everygist pamoja na
afisa kilimo wa kituo cha Mwamala Simon Bitege wanaelezea ukubwa wa tatizo hilo
Chapisha Maoni